Klabu bingwa

Klabu bingwa ya ni Raja au Bayern? Timu ya Raja Casablanca kutoka Morocco imefuzu kucheza fainali za klabu bingwa ya dunia baada ya kuisambaratisha Atletico Mineiro kutoka Brazil katika mchezo wa nusu fainali. Raja waliweza kufunga magoli mawili katika dakika 10 za mwisho katika mchezo huo. Taarifa zinazohusiana FIFA , Kandanda Kwa matokeo hayo Raja Casablanca watamenyana na Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa fainali. Raja ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao lililofungwa na Mouhssine Lajour. Mchezaji wa zamani wa Barcelona Ronaldinho alipiga kiufundi mpira wa adhabu na kuisawazishia bao timu yake ya Mineiro. Lakini Mohaine Moutaouali aliiweka mbele timu yake ya Raja baada ya kufunga mpira wa penalti, huku Vivien Mabide akikamilisha ushindi wa magoli 3 ya Raja dhidi ya 1 la Mineiro. Kivutio katika mchezo ni kwa wachezaji wa Raja kumzunguka Ronaldinho mara baada ya kupigwa filimbi ya kumaliza mchezo, huku wakimbusu na jezi na viatu vyake kam...