Ghana yapiga marufuku majokofu mitumba
Serikali ya Ghana imepiga marufuku uagizaji wa majokofu yaliyotumika au mitumba ili kupunguza matumizi ya nishati na uchafuzi wa mazingira. Wafanyabiashara wa majokofu Ghana Majokofu mengi kukuu yana kemikali inayoitwa Chlorofluorocarbons (CFCs) inayoharibu mazingira. Licha ya kuwa bidhaa hizo zimepigwa marufuku, na hazitengenezwi tena, majokofu hayo yanaaminika kutumika barani Afrika. Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Nishati ya Ghana ameimbia BBC kuwa marufuku hiyo, imelifanya taifa lao kuwa kielelezo katika kanda ya Afrika Magharibi. Sheria ya kupiga marufuku majokofu hayo iliidhinishwa mwaka wa 2008, lakini muda wake uliongezwa ili kuwa na wauzaji wa bidhaa hizo kufanya marekebisho. Hata hivyo wafanyabiashara kadha nchini Ghana wameshutumu uamuzi huo wa serikali wakisema idadi kubwa ya watu watak...