Mzozo kuhusu tuzo ya CECAFA
Mchezaji wa Uganda akikabiliana na mchezaji wa Kenya Mshambulizi wa timu ta taifa ya soka ya Uganda Cranes, Uganda, Robert Ssentongo, ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya CECAFA Tusker Senior Challenge Cup, yaliyomalizika mjini Kampala. Sentongo hata hivyo alifunga magoli manne pekee wakati wa mashindano hayo. Wachezaji waliofunga idadi magoli mengi kuliko Sentongo,Mrisho Ngassa na John Bocco wa timu ya Tanzania bara, walinyimwa tuzo hilo, na kamati ya ufundi ya mashindano hayo. Katika mashindano yaliyopita, mchezaji aliyefunga idadi kubwa ya magoli ndiye huibuka mshindi wa taji hilo, lakini mwaka huu mambo nchini Uganda yalikuwa tofauti. ''Ngassa na Bocco walifunga magoli matano kila mmoja na ilitarajiwa wangepewa tuzo ya mfungaji bora lakini katika hali ya kushangaza kamati ya CECAFA, ilimpa tuzo hilo mshambuliaji wa Uganda, Robert Ssentongo aliyefunga magoli manne'' Alisema kocha wa Kilimanjaro Stars. Katibu mkuu wa CECAFA akiwa na kome ...