Jee unajua kuwa ukikua pua yako na masikio yako pia yanazidi kukua , kurefuka na kupanuka? Hebu angalia wazee walio karibu na wewe utaona kuwa pua zao ni ndefu au zimepanuka. Masikio yao pia ni marefu. Ni sayansi hiyo! Jee unajua kuwa macho peke yake ndio hayakui? Tangu ulipozaliwa hadi sasa macho yako, yako vile vile, ukubwa ule ule. Macho hayapanuki wala hayakui! Mifupa ya Maiti Kitandani ...... Kwanini basi masikio na pua vinakua? Ukweli ni kwamba vyote havikui. Pua haikui, masikio pia hayakui. Isipokuwa vyote vinavutika! Pua na masikio huvutika vikielekea chini kadri umri unavyoongezeka! Wanasayansi wanasema hii ni kutokana na nguvu ya mvuto au Force of Gravity, Mvuto wa kuelekea ardhini, Force of Gravity! Hii nguvu ya mvuto kuelekea ardhini au force of gravity ni mbaya sana! Nguvu hii ya asili ndio hufanya , nyama mwilini ikavutika au kusinyaa na macho kuonekana madogo. Ukubwa wa macho ni ule ule bali yanaonekana madogo kwa sababu yameingia ...
Comments
Post a Comment