Balotelli kupinga uamuzi wa Man City
- Get link
- X
- Other Apps

Mario Balotelli akipewa kadi nyekundu wakati wa mechi yao na Arsenal
Mshambulizi wa Manchester City Kutoka Italia, Mario Balotellu, atafika mbele ya kamati maalum ya shirikisho la mchezo wa soka nchini England siku ya Jumatano.
Balotelli anapinga uamuzi wa klabu yake ya Manchester City ya kumpiga faini ya mshahara wake wa wiki mbili kuhusiana na rekodi yake mbovu ya nidhamu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, alikosa mechi 11 za ligi kuu na michuano ya ulaya msimu uliopita.
Balotelli alikata rufaa kuhusu aumuzi huo, lakini kamati huru ya wanachama wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo wakaifutilia mbali.
Balotteli anatarajiwa kufika mbele ya kikao hicho binfasi, pamoja na wakili wake kutoka Italia na mwakilishi mmoja wa chama cha wachezaji wa kulipwa, huku klabu ya manchester City ikialishwa na mawakili wake.
Je Balotelli anastahili faini hiyo?

David Bernstein mwenyekiti wa FA
Faini hiyo ndicho kiwango cha juu zaidi kuambatana na kandarasi ya wachezaji, lakini klabu ya Manchester City imekataa kuzungumzia suala hilo na wanamatumaini makubwa kuwa jopo hilo litafutilia mbali, rufaa hiyo.
Ni nadra sana kuona masuala ya ndani kati ya vilabu na wachezaji wao yalifika mbele ya kamati hiyo maalum.
Chama cha wachezaji wa soka wa kulipwa PFA, kimekuwa kikitoa ushauri kwa Balotelli tangu mzozo huo kuanza na afisa wake mkuu mtendaji Gordon Taylor, ameiambia BBC kuwa ''Tunajaribu kadri ya uwezo wao kuzuia masuala kama hayo kufika mbele ya kamati hiyo ya FA, lakini kwa kuwa mchezaji huyo na klabu yake hawajaafikiana''.
Klabu hiyo ilianzisha uchunguzi kuhusiana na mchezaji huyo baada ya kupewa kadi nyekundu wakati wa mechi yao dhidi ya Arsenal Aprili mwaka huu.
Kwa ujumla, Belotelli amepewa kadi za njano tisa na tatu nyekundu.
Balotelli aliondolewa katika kipindi cha pili wakati wa mechi yao dhidi ya Manchester United ambapo walishindwa kwa magoli 3-2 tarehe 9 mwezi huu, na kisha kuachwa nje ya kikosi cha mabingwa hao watetezi wakati wa mechi yao dhidi ya Newcastle ambayo walishinda kwa magoli 3-1.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment