England yailemea India

Wachezaji wa Kriketi wa England

Wachezaji wa Kriketi wa England
Wachezaji wa Kriketi wa England
England imekamilisha ushindi wake wa kwanza katika mashindano ya Kriketi kwa zaidi ya miaka 27 nchini India, huku wachezaji wawili wa Uingereza Jonathan Trott na Ian Bell wakiandikisha zaidi ya mikimbio mia mmoja kila mmoja katika mechi hiyo iliyochezwa mjini Nagpur.
Trott aliweka mikimbio 143 naye Bell alipata 116 na kusalia hadi mwisho wa pambano hilo nna kuruhusu wenyeji wao India ambao walishindwa mjini Ahmedabad na kushinda mechi za Mumbaina Kolkata kupata sare iliyohitajika kuhakikisha ushindi wa England.
India ilifanikiwa kumuondoa mchezaji mmoja tu wa England siku nzima na kutoa nafasi kwa Joe Root kucheza mechi yake ya kwanza na kuweka mikimbio 20.
Awali England ilimaliza ikiwa na mikimbo 356 zaidi baada ya mchuano huo kumalizika huku wakiwa na mikimbio 352 baada ya kuwapoteza wachezaji wanne.
Wachezaji wa England wanasema ushindi huo ulikuwa muhimu sana kwa kuwa walishindwa kwa wiketi tisa katika mechi yao ya kwanza lakini tangu wakati huo, wamefanikiwa kuwashinda wenyeji wao katika idara zote.
Licha ya kuwa England ilishinda mashindano ya Kriketi ya Ashes, baadhi ya wachezaji wa zamani wa England akiwemo naodha wa zamani Michael Vaughan amesema kushinda mchuano wa kriketi dhidi ya India wakiwa nyumbani ni jambo gumu sana.
Ushindi huo ni wa nne kwa England nchini India na ni ya kwanza tangu kikosi kilichoongozwa na David Gower kushinda mwaka wa 1984-85.
England vile vile imefutilia mbali rekodi ya India ya kutoshindwa nyumbani tangu mwaka wa 2004, wakati Australia ilipoiadhibu mbele ya mashabili wake.

Comments

Popular posts from this blog

FIELD REPORT ON BTCIT 2012

Afanya mapenzi na mifupa ya maiti