Demba Ba kuhama Newcastle

Mchezaji wa Newcastle Demba Ba
Alan Pardew yuko tayari
kumsajili mshambulizi wa Ukraine Artem Milevskiy ikiwa nyota wake Demba
Ba hatasaini mkataba mpya na klabu hiyo.
Kocha huyo wa Newcastle ameshindwa kumshawishi Demba Ba kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.Klabu hiyo sasa inashauku nyingi kuhusiana na kipengee katika mkataba wake unaosema klabu yoyote inayotaka kumsajili mchezaji huyo kabla ya muda wake kumalizika ni sharti ili pauni milioni saba ikiwa atakihama klabu hiyo mwezi Januari mwakani.
Pardew anafahamu wazi kuwa haitagharimu klabu yake hela nyingin kumsajili Milevskiy, 27, kutoka kwa klabu ya Dynamo Kiev.
Klabu hiyo iliitisha pauni milioni 14 wakati Roy Hodgson alipojaribu kumsajili mchezaji huyo akiwa na klabu ya liverpool.
Comments
Post a Comment