Kocha amtaka Adebayor kubadili uamuzi

Emmanuel Adebayor
Emmanuel Adebayor akizungumza na refa
Kocha wa Togo Didier Six amesema atafanya kila juhudi ili kumshawishi mshambulizi wa Tottenham, Emmanuel Adebayor kuichezea timu ya taifa ya Togo wakati wa michuano ya kombe la Mataifa bingwa Barani Afrika, mwezi ujao.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 28, alitangaza kustaafu kutoka kwa kechi zote za kimataifa, kwa sababu ya mzozo wake na shirikisho la mchezo wa soka, kuhusiana na malipo ya ziada.
Six alisema'' nafanya kila juhudi ili niweze kumshawishi abadili uamuzi wake''
''Yeye ni mchezaji wa hadhi ya juu na pia naodha wa timu yetu ya taifa. Adebayor ana jukumu kubwa kwa kikosi chetu'' aliongeza kocha huyp huyo.
Msemaji wa mchezaji huyo, Amedodji Blaise mapema mwezi huu alisema
Adebayor hatashiriki katika mechi yoyote ya kimataifa kwa muda usiojulikana na hatashiriki katika michuano hiyo ya bara la Afrika.
Huku tangazo la Adebayor likiwa pigo kubwa kwa timu ya Taifa ya Togo, habari hizo zilipokelewa vyema na klabu yake ya Tottenham, ambayo haitaki kukosa huduma za mchezaji huyo wakati muhimu wa ligi.
Ikiwa Togo itafanikiwa kumshawishi adebayor, basi huenda akakosa mechi ya Tottenham dhidi ya QPR, Manchester United, Norwich, West Brom na Newcastle.
Togo inashiriki katika fainali hizo za Arika kwa mara ya kwanza tangu ilipojiondoa kutoka kwa fainali ya mwaka wa 2010 nchini Angola, baada ya basi lao kushambuliwa na magaidi.

Comments

Popular posts from this blog

FIELD REPORT ON BTCIT 2012

Afanya mapenzi na mifupa ya maiti